Chelsea yatangaza namba watakazovaa Kepa na Kovacic - Darajani 1905

Chelsea yatangaza namba watakazovaa Kepa na Kovacic

Share This

Kuelekea msimu mpya wa 2018-2019, nyota hawa watavaa jezi zenye namba hizi.

Kepa Arrizabalaga aliyesajiliwa kwa kuvunja rekodi ya usajili wa kipa ghali zaidi duniani atavaa jezi nambari 1 ambayo kabla ilikuwa ikivaliwa na Willy Caballero hivyo kumaanisha Caballero atavaa jezi namba 13 iliyoachwa na mlinda mlango Thibaut Courtois.

Kwa upande wa Mateo Kovacic, atavaa jezi namba 17 wakati Ruben Loftus-Cheek atavaa jezi namba 14 ambayo kabla ilikuwa ikivaliwa na Tiemoue Bakayoko ambaye anaweza kuondoka kwa mkopo.

Alvaro Morata atavaa jezi namba 29 tofauti na kabla alipokuwa akivaa jezi nambari 9. Aliamua kuvaa jezi namba 29 kutokana na furaha aliyokuwa nayo kwa watoto wake mapacha waliozaliwa tarehe 29-Julai mwaka huu.

No comments:

Post a Comment