Rasmi; Wengine wawili wa Chelsea waondoka kwa mkopo - Darajani 1905

Rasmi; Wengine wawili wa Chelsea waondoka kwa mkopo

Share This

Nyota wawili wa Chelsea wamekamilisha uhamisho wa kuondoka Chelsea na kujiunga na klabu za Everton ya nchini Uingereza na mwengine akijiunga na klabu ya Valencia ya nchini Hispania

Kurt Zouma amekamilisha usajili wa kujiunga kwa mkopo na klabu ya Everton ambayo kocha wake, Marco Silva alisema kabla ya usajili huo kukamilika kwamba ilibakiza hatua za mwisho kumnasa nyota huyo raia wa Ufaransa ambaye msimu uliopita aliichezea kwa mkopo klabu ya Stoke city ambayo baadae ilishuka daraja.

Wakati Zouma akikamilisha uhamishho huo, nyota mwengine anayecheza nafasi ya ushambuliaji, Michy Batshuayi naye amekamilisha uhamisho wa kujiunga kwa mkopo nak klabu ya Valencia inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania.

No comments:

Post a Comment