Nini hatma ya Bakayoko kuhusu kuondoka Chelsea? - Darajani 1905

Nini hatma ya Bakayoko kuhusu kuondoka Chelsea?

Share This

Mpaka kufungwa kwa dirisha la usajili hapo jana mida ya saa 19:00 kwa saa za Afrika Mashariki bado hakukuwa na taarifa kamili kuhusu uhamisho wa mkopo wa kiungo wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko ambaye alikuwa akihusishwa kutakiwa na klabu kadhaa zikiwemo klabu za jiji moja huko jijini Milan nchini Italia, Inter Milan na AC Milan.

Kwa taarifa za mwisho kuhusu nyota huyo zinadai kwamba Chelsea ilikuwa tayari kumtoa nyota huyo kwa mkopo wa msimu mzima uku ikikubali kiwepo kipengele cha kusajiliwa jumla endapo klabu hiyo ikimtaka na kuridhishwa nae lakini tatizo likaja kwenye mshahara wa nyota.

Ipo hivi, Chelsea ilitaka kama klabu atakayoenda ikimtaka jumla mara baada ya kucheza kwa mkopo kwa msimu mzima basi italazimika kutoa paundi milioni 30 ili kumsajili jumla, kumbuka Chelsea ilimsajili kwa paundi milioni 40 kwahiyo ilikuwa tayari kupata hasara ya paundi milioni 10 lakini wakati mazungumzo yakiwa yanaendelea kati ya Chelsea na AC Milan waliokuwa wanamfukuzia kwa karibu kikwazo kikaja kwenye mshahara wa nyota huyo.

Chelsea inamlipa paundi milioni 5.8 kwa mwaka, mshahara ambao AC Milan wameona mkubwa kwao kumlipa kiungo huyo kwa mwaka na wakaiomba Chelsea iwe inaendelea kumlipa mshahara (wote au nusu) wakati akiwa bado kwa mkopo.

Kwa kawaida klabu huwa zinakubaliana juu ya mchezaji aliye kwa mkopo kama klabu iliyomtoa kwa mkopo itaendelea kumlipa mshahara wote au klabu mbili zitagawana kiasi flani ili wamlipe.

Ila usajili umefungwa kwa Uingereza tu lakini kwa ligi kuu za nchi nyengine wanaruhusiwa kusajili na kuuza ila klabu za Uingereza haziruhusiwi kusajili ila zinaruhusiwa kuuza.

No comments:

Post a Comment