Chelsea yajiandaa kuvunja rekodi kwa Lewandowski - Darajani 1905

Chelsea yajiandaa kuvunja rekodi kwa Lewandowski

Share This

Klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza inatajwa kuwania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich ambaye ni raia wa Poland, Robert Lewandowski huku ikipambana dhidi ya Real Madrid ambayo nayo inamhitaji mshambuliaji huyo.

Nyota huyo anadaiwa kukiri anatamani kuondoka kwenye klabu hiyo ya nchini Ujerumani ili kutafuta changamoto mpya kwenye klabu nyengine tofauti na inayoshiriki ligi ya nchini humo, ligi ya Bundesliga.

Chelsea inatajwa kumuwania mshambuliaji huyo huku ikiwa imeandaa dau litakalovunja rekodi ya dau kubwa kutumika kwenye usajili nchini Uingereza ambayo mpaka sasa inashikiliwa na kiungo wa Manchester united, Paul Pogba ambaye usajiki wake uligharimu paundi milioni 87 wakati kwa upande wa Chelsea imeandaa paundi milioni 100 ili kumnasa mshambuliaji huyo mwenye miaka 29 kwa sasa.

No comments:

Post a Comment