Abramovich kuiuza Chelsea - Darajani 1905

Abramovich kuiuza Chelsea

Share This

Siku moja baada ya Chelsea kutwaa taji la kombe la FA ikiibamiza klabu ya Manchester united kwenye fainali ya kombe hilo iliyochezwa pale kwenye uwanja wa Wembley uliopo jijini London kulitoka taarifa juu ya kibali cha kuishi nchini Uingereza cha mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kuwa kimeisha. Ili kuisoma taarifa hii kwa undani zaidi, bonyeza hapa.

Lakini kumeibuka habari na taarifa mpya ambayo hii inatajwa kuwa mbaya kwa klabu na wapenzi pamoja na mashabiki wa Chelsea.

Taarifa iliyochapishwa na chombo fulani nchini Uingereza kinadai mmiliki huyo anaweza akaiuza klabu hiyo ya Chelsea licha ya kudumu nayo toka mwaka 2003 alipoinunua kutoka kwa Ken Bates.

Mmiliki huyo anatajwa kutopendezwa jinsi mwenendo wa Chelsea ulivyo kwa sasa lakini pia kumalizika kwa kibali cha muda wake wa kuishi nchini Uingereza kunachochea mpango wake wa kuiuza klabu hiyo.

Moja ya waalimu wa maswala ya fedha katika soka (Football Finance) kwenye chuo kikuu kinachopatikana Liverpool anadai mpango huo wa kuiuza Chelsea utaifanya klabu hiyo kuwa kwenye wakati mgumu haswa kutokana na mpango wake wa kuutanua uwanja wake wa Stamford Bridge ambapo inahitaji kiasi cha paundi bilioni 1 ili iweze kukamilisha ujenzi huo wa uwanja huo ambao kwa sasa unaingiza mashabiki 40,000 lakini kama upanuzi ukikamilika basi utaweza kuchukua mashabiki 60,000

Wasiwasi uliopo je huyo atakayeuziwa klabu hiyo atakubali kutoa kiasi hicho ili kukamilisha upanuaji wa uwanja huo ambao unatarajiwa kuanza mwishoni mwa msimu ujao. Hilo halionekani kuwezekana maana dau atakalolilipa ili kuinunua klabu hiyo litakua ni zaidi ya dau atakalotumia kuujenga uwanja huo.

No comments:

Post a Comment