Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea imefanikiwa kucheza mchezo wake wa mwisho wa ligi kuu jioni ya leo ambapo ilisafiri mpaka kwenye uwanja wa Preston Park unaomilikiwa na klabu ya soka ya wanawake ya Liverpool na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-3 dhidi ya klabu hiyo.
Chelsea Ladies ambayo ilishakuwa mabingwa wa ligi hiyo maarufu kama FA WSL (Football Association Women Super League) ambapo ilitawazwa rasmi kuwa mabingwa kwenye mchezo uliopita walipomenyana dhidi ya Bristol city walishuka uwanjani jioni ya leo na kucheza dhidi ya madada wa Liverpool ambao waliweza kuitangulia magoli mawili katika kipindi cha kwanza na kufanya mchezo kwenda mapumziko huku Chelsea Ladies wakiwa nyuma kwa magoli mawili kwa sifuri.
Kipindi cha pili kilionekana kizuri kwa Chelsea Ladies ambapo hawakutaka kufanya makosa. Eni Aluko, mdada mwenye asili ya Afrika huko magharibi mwa bara hilo lakini akiitumikia timu ya taifa ya Uingereza ambapo huko ndipo alipolelewa na kukulia akaifanya Chelsea Ladies irudishe hali ya ushindi mara baada ya kusawazisha goli la kwanza.
Ji So-Yun, mwanadada raia wa Korea anayecheza nafasi ya kiungo mwenye uwezo mkubwa wa kufunga akaisawazishia tena Chelsea goli la pili na kuifanya mchezo kuwa sare ya 2-2 lakini tena wakati mpira ukionekana kuelekea mwishoni, Ji tena akaifungia goli la tatu na kuifanya Chelsea Ladies kushinda mchezo huo kwa mabao 2-3 huku ikiwa ugenini.
Kwa matokeo haya yanaifanya Chelsea kutwaa ubingwa wa ligi kuu hiyo ya wanawake bila kupoteza mchezo wowote huku Fran Kirby akiibuka mfungaji na mchezaji bora wa ligi hiyo na hata kwa upande wa klabu.
No comments:
Post a Comment