Jana ilikuwa ni siku tamu kwa kila shabiki na mpenzi wa klabu ya Chelsea mara baada ya klabu hiyo kutwaa taji la kombe la FA ikiibamiza Manchester united kwa goli 1-0 lililofungwa kwa mkwaju wa penati na winga wake Eden Hazard.
Lakini katika mchezo huo kuliibuka gumzo juu ya mmiliki wa klabu hiyo ya Chelsea, Roman Abramovich ambapo hakuonekana kabisa kwenye mchezo huo ambapo hiyo sio kawaida yake haswa Chelsea inapocheza mchezo wa fainali au ikiwa inakabidhiwa kombe au taji lolote.
Baada ya kufanyika utafiti kwa kiasi kikubwa jibu likapatikana kuwa mmiliki huyo ambaye ni raia wa Urusi amerejea nchini kwao mara baada ya kibali (visa) ya kuishi nchini Uingereza kumalizika toka mwezi Aprili mwaka huu.
Chanzo cha habari kinadai mmiliki huyo ambaye alianza kuishi nchini Uingereza toka mwaka 2003 alipoinunua Chelsea kutoka kwa Ken Bates amekua akiishi nchini humo na kibali chake kimekamilika au kuisha mwezi Aprili mwaka huu. Taratibu za kuomba kibali kingine zinatajwa tayari kufanyika ila ugumu unaletwa juu ya mgogoro uliopo kati ya nchi yake ya Urusi na nchi Uingereza. Mmiliki huyo anatajwa kuwa na utajiri wa paundi bilioni 9.3
No comments:
Post a Comment