Paundi milioni 32 na mkataba wa miaka mitano ulimfanya nyota raia wa Ufaransa, N'golo Kante atuea Chelsea rasmi akitokea klabu iliyochini ya tajiri wa kiasia, klabu ya Leicester city.
Kutua kwake Chelsea ni kama kulisaidia maana kuliifanya Chelsea itoke ilipomaliza msimu uliopita wa 2015-2016 ambapo ilimaliza katika nafasi mbaya katika msimamo wa ligi kuu Uingereza lakini ujio wake pamoja na kocha Antonio Conte ni kama ukarudisha uimara wa Chelsea na kufanikiwa kushinda taji la ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2016-2017 huku nyota huyo mwenye asili ya Afrika kutoka nchi ya Mali akishinda tunzo kadhaa huku akitajwa kati ya viungo bora kwa sasa.
Mtindo wake wa uchezaji umekuwa ukiwafurahisha wengi mpaka baadhi kufikia hatua kumpachika jina la kiumbe 'Kicheche' ambaye anasifa ya ujanja mwingi na ukabaji wa kipekee.
Leo anatimiza miaka 27 toka kuzaliwa kwake mwaka 1991.
Jambo ambalo huenda hulijui, nyota huyu alishawai kukiri kama asingekuwa mwanasoka basi angekuwa mchezaji wa mchezo wa'rugby'
Hongera N'golo Kante
No comments:
Post a Comment