Chelsea itakuwa nyumbani mwisho wa wiki hii ili kucheza mchezo wake wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Tottenham katika uwanja wa Stamford Bridge, mchezo ambao Chelsea italazimika kupata ushindi ili ijiweke katika nafasi nzuri ya kugombania kwake kuingia kwenye klabu nne za juu katika msimamo wa ligi kuu.
Chelsea kwa sasa imeachwa alama tano na Tottenham inayoshika nafasi ya nne huku Chelsea ikiwa nafasi ya tano, lakini kuelekea kwenye mchezo huo, gwiji na nahodha wa zamani wa Chelsea anaamini Chelsea ni lazima itaiadhibu klabu hiyo ambazo zote zinapatikana kwenye jiji moja nchini Uingereza, jiji la London.
Gwiji huyo anaamini Chelsea itaendeleza rekodi yake safi iliyokuwa nayo dhidi ya klabu hiyo ya Tottenham ambapo toka mwaka 1990 mpaka kufikia hii leo, klabu ya Tottenham haijawai kushinda mchezo wowote dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge na mwisho wa wiki hii gwiji huyo anaamini Chelsea itaendeleza ubabe huo kwa kupata ushindi mnono.
No comments:
Post a Comment