Chelsea imeachana na Luis Enrique, je unajua sababu? - Darajani 1905

Chelsea imeachana na Luis Enrique, je unajua sababu?

Share This

Klabu ya Chelsea ilikuwa ikitajwa kumfukuzia kocha wa zamani wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania, Luis Enrique ili arithi nafasi ya kocha wa sasa klabuni Chelsea, Antonio Conte ambaye amekua akitajwa kuondoka klabuni hapo. Lakini sasa dili hilo linaonekana kuzikwa na kufutika kabisa, je unajua sababu ni nini?

Gazeti moja la nchini Hispania limeandika moja ya viongozi klabuni Chelsea ambaye ni kiongozi mkuu kwenye bodi ya klabu hiyo huku akiwa na majukumu ya usajili klabuni hapo alisafiri na kukutana na kocha huyo lakini mazungumzo baina yao hayakufikia mwisho mzuri.

Kutokuelewana kwao kumemfanya mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich ameshindwa kupitisha uamuzi juu ya kocha huyo kutua Chelsea huku kocha wa Napoli, Maurizio Sarri akitajwa pia kwa karibu kutua Chelsea kama mbadala wa Antonio Conte.

No comments:

Post a Comment