Heri ya kuzaliwa Petr Cech - Darajani 1905

Heri ya kuzaliwa Petr Cech

Share This

Leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mchezaji nyota wa zamani wa Chelsea, Petr Cech ambaye kwa sasa ni mlinda mlango wa klabu ya Arsenal ambayo alijiunga nayo mwaka 2015.

Alisajiliwa na Chelsea akitokea klabu ya Rennes hiyo ikiwa ni mwaka 2004 na tangu ajiunge na Chelsea amefanikiwa kutwaa mataji na kuweka rekodi kibao kwa soka la ligi kuu Uingereza haswa akiwa mlinda mlango wa klabu bora, klabu ya Chelsea.

Alikuwa ndiye mlinda mlango wa kwanza kumaliza michezo 100 bila kuruhusu kufungwa goli ambapo alifanya hivyo katika michezo 108 tu huku akiitumikia Chelsea kwa michezo 408. Kaisaidia Chelsea kushinda ligi kuu Uingereza, klabu bingwa barani Ulaya maarufu kama Uefa Champions League, kombe la ligi la Ulaya (Europa League), kombe la ligi pamoja na kombe la FA kabla ya kuachana na Chelsea mwaka 2015.

Lakini je wajua kwanini anavaaga kofia? sababu ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Reading mwaka 2006 akiwania mpira dhidi mchezaji wa Reading, Stephen Hunt na ndipo Cech akagongwa kichwani na mshambuliaji huyo na akajaribu kufanyiwa matibabu kwa muda mrefu ila ikaonekana majanga mpaka alipotolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Carlo Cudicini ambaye naye aliumia na ikambidi John Terry avae nguo hizo za makipa.

Heri ya kuzaliwa, miaka 36

No comments:

Post a Comment