Makala; Sababu hii nayo imeifanya Chelsea ifanye vibaya - Darajani 1905

Makala; Sababu hii nayo imeifanya Chelsea ifanye vibaya

Share This

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte alitua klabuni hapo akitokea kwenye mashindano ya Euro pindi alipokua kocha wa timu ya taifa ya Italia. Wengi hawakumfahamu sana licha ya kuiongoza vyema klabu ya Juventus kutwaa mataji kadhaa nchini Italia. Hakuna aliyetegemea kama kocha huyo angefanya makubwa kwa Chelsea iliyotoka kumaliza kwenye nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza pindi ilipokua chini ya kocha Jose Mourinho aliyemwachia Guus Hiddink amalize nayo msimu.

Wachambuzi wengi walimtabiri Conte kuwa moja ya makocha watakaoshindwa kuirudisha Chelsea kwenye ramani na ushindani wa kushinda mataji. Hakuna aliyeliwaza hilo. Hata kocha wa zamani wa Manchester united, Sir. Alex Fabregas hakuipa Chelsea kwenye nafasi nne za juu pindi ligi hiyo itakapomalizika.

Lakini makubwa aliyoyafanya yalistaajabisha dunia ambapo aliutumia ufundi na uchawi wa mfumo wake wa 3-4-3 kushinda taji la ligi kuu Uingereza lakini pia kuifanya Chelsea ifudhu kucheza klabu bingwa Ulaya lakini pia ikifanikiwa kufika fainali ya kombe la FA ambapo ilipoteza dhidi ya Arsenal.

Lakini je unazani ni kipi kilitarajiwa kwa kocha huyo kukifanya kwa msimu wake wa pili? bila shaka kwa rekodi mpya alioiweka kwenye msimu wake ya kushinda michezo 31 kwa msimu mmoja (kwa sasa imevunjwa na Man city) bila shaka yalitegemewa makubwa kutoka kwake.

Chelsea ikafanikiwa kurejea klabu bingwa ila pia ikiwa inashindania mataji 4 ukiachana na lile la ngao ya hisani ambalo Chelsea ilipoteza tena mbele ya Arsenal.

Lakini msimu wake wa pili ukawa mbaya japo amejinusuru kidogo kwa kufanikiwa kutwaa taji la kombe la FA. Ila kombe hilo moja haibadilishi kuwa Chelsea haijawa kwenye hali nzuri msimu huu. Imeshindwa kumaliza kwenye nafasi nne za juu na kushindwa kukata tiketi ya kushiriki michuano hiyo ya Ulaya kwa msimu ujao.

Kuna sababu nyingi zinatajwa kuifanya Chelsea ishindwe kufanya vizuri msimu huu lakini hapa nakuletea moja ya sababu hizo.

Kocha Antonio Conte anaonekana kuwa tatizo juu mahusiano yake binafsi kati yake na wachezaji lakini pia kati yake na benchi lake la ufundi.

Diego Costa alikuwa ni kipenzi cha kila mchezaji klabuni Chelsea, alikuwa ni rafiki wa wachezaji wote makudhi na utani wake kwa kila mchezaji kulimfanya kuwa na nguvu kubwa ya ushawishi wa wachezaji wenzake. Mgogoro wake na kocha Antonio Conte kulimfanya aondoke klabuni hapo huku akikubali kutocheza kwa nusu msimu wote akiisubiri Atletico Madrid itoke kwenye kifungo cha kutokusajili ili ajiunge nayo. Kuondoka kwake kuliwadhoofisha wachezaji na hakuna aliyependa kutengana na mshambuliaji huyo ambaye alisaidia kwa kiasi kikubwa kuifanya Chelsea kutwaa taji la ligi kuu katika msimu uliopita wakati Conte akiifundisha Chelsea kwa msimu wa kwanza. Lakini wakati Conte akifanya kazi nchini Uingereza kwa mara ya kwanza.

David Luiz ni moja kati ya wachezaji wenye ushawishi mkubwa klabuni Chelsea, na wengi waliamini angeweza kuwa mrithi wa unahodha kutokq kwa John Terry. Kinda wa Chelsea, Andreas Christensen alishawai kukiri mchezaji huyo anaushawishi mkubwa akiwa kama nahodha wa klabu huku akionekana kuwa kiongozi kuliko hata Gary Cahill ambaye ndiye nahodha mkuu.

Lakini mgogoro kati yake na kocha Antonio Conte unatajwa kuibuka toka kocha Conte alipokua kwenye mgogoro na Diego Costa ambapo inarlezwa David Luiz alikuwa akihusika kama mpatanishaji. Amecheza michezo michache msimu huu huku kocha akidai majeraha aliyoyapata alipochezewa vibaya na Kun Aguero ndio yanamfanya kukaa nje kwa musa mrefu.

Chanzo kingine kinadai wawoli hao wapo kwenye mgogoro uliosababishwa baada ya mchezo wa ugenini wakati Chelsea ilipocheza dhidi ya As Roma na kupoteza kwa magoli 3-0 huku David Luiz akicheza chini ya kiwango huku akikataa lawama alizolaumiwa na kocha Conte na toka mchezo huo amekua akitumikia benchi kwa muda mrefu.

Ugomvi kati yake na bodi ya Chelsea. Amekuwa akilalamika sana kwenye vyombo vya habari juu ya kutopewa mamlaka kamili juu ya ufanyaji usajili klabuni hapo lakini kama hilo haliroshi ikafikia kipindi ikaripotiwa kocha huyo anaonga na mtu mmoja tu klabuni hapo ambaye ni kaka yake aliyetoka nae nchini Italia na kumfikisha klabuni hapo kama moja ya watu lwenye benchi la ufundi.

Ilielezwa kocha huyo amekua hana mahusiano mazuri na viongozi klabuni Chelsea mpaka kufikia hatua kukata mawasiliano na viongozi hao. Unadhani unaweza kufanikiwa kwa mgogoro na viongozi wanaoisimamia klabu yako na hata we mwenyewe.

Winga wa Chelsea, Willian Borges da Silva aliwai kuulizwa juu ya mahusiano yake pamoja na kocha huyo ambapo alianza kwa kucheka na kusema swali hilo atalijibu siku nyengine. Unazani kuna nini hapo kati?

David Luiz hakumualika kocha Antonio Conte kwenye sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa nyota huyo, unazani kuna nini hapo kati?

No comments:

Post a Comment