Zimesalia siku kadhaa ili kuanza kwa michuano ya kombe la dunia kwa mwaka 2018, michuano itakayochezwa huko nchini Urusi.
Kuelekea kwenye michuano hiyo timu kadhaa za taifa zimeshatangaza vikosi vya wachezaji wake 23 ambao wataungana kwa kila timu ili kushiriki michuano hiyo itakayoanza mwezi Juni mwaka huu.
Timu ya taifa ya Ubelgiji nayo imekitangaza kikosi chake hiko cha wachezaji 23 ambapo ndani yake kuna wachezaji watatu wa Chelsea.
Eden Hazard, mlinda mlango Thibaut Courtois pamoja na mshambuliaji Michy Batshuayi ambaye ameicheza kwa mkopo klabu ya Borrusia Dortmund ambapo huko ameonyesha ubora wa hali ya juu.
Hongereni nyota wetu...
No comments:
Post a Comment