Nadhani unakumbuka kauli iliyotolewa na winga wa Chelsea, Eden Hazard akisema sababu itakayomfanya aendelee kusalia klabuni hapo licha ya kutakiwa na klabu kadhaa zikiwemo Real Madrid na Manchester city. Kusoma alichokisema, bonyeza hapa
Nyota huyo ametoa kauli nyengine mpya kuhusu hatma yake ya kuendelea kusalia Chelsea.
"Klabu ina wachezaji wazuri, wachezaji wenye uwezo mkubwa. Ni jambo zuri kucheza na wachezaji wenye hali ya ushindi. Kama klabu pamoja na wachezaji wanalengo moja tu wanalolitazama kwa pamoja, ni kushinda kila aina ya taji. Naamini ata wakisajiliwa wachezaji wapya basi inabidi tuwaambie klabu nini inataka. Inataka mataji" alisema winga huyo mwenye miaka 27 kwa sasa ambapo kwa kauli yake inaonekana kutamani kusalia klabuni Chelsea ambapo alitua mwaka 2013 akitokea Lille ya Ufaransa.
Klabu za Real Madrid na Man city zimekua zikiwania saini yake ila Chelsea haionekani kutamani kuachana na nyota huyo huku ikijaribu mara kadhaa kumsainisha mkataba mpya huku likiandaliwa dau la mshahara la kufikia paundi 300,000 kwa wiki.

No comments:
Post a Comment