Rasmi; Chelsea yatwaa ubingwa wa FA, Mtafuteni Manara aje aseme "This is Chelsea" - Darajani 1905

Rasmi; Chelsea yatwaa ubingwa wa FA, Mtafuteni Manara aje aseme "This is Chelsea"

Share This

Chelsea inafanikiwa kuondoka na ubingwa wa kombe la FA mara baada ya kuitandika Manchester united kwa goli 1-0 lililofungwa na Eden Hazard kwa mkwaju wa penati.

Mchezo kwa ufupi; Chelsea ilianza kipindi cha kwanza ikionekana kukamia mchezo huku ikitengeneza mashambulizi mengi kabla ya kupata goli moja na la ushindi likifungwa na Eden Hazard, penati iliyopatikana kwa mlinzi wa Manchester united, Phil Jones kumchezea vibaya Hazard kwenye eneo la hatari. Goli hilo likifungwa dakika ya 22.

Kipindi cha pili kilikuwa upande wa Manchester united ambao walijaribu kutengeneza mashambulizi mengi ambayo hayakuzaa matunda ambapo safu ya ulinzi ya Chelsea ilionekana kuwa imara zaidi.

Kidunchu; Kwa ushindi huu sasa kocha Antonio Conte anafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Manchester united iliyochini ya kocha Jose Mourinho kwenye michezo 4 kati ya sita ilizomenyana klabu hizo. Tangu Conte awe kocha wa Chelsea. Ukidunchu mwengine kama haujui hili ndilo taji pekee la FA kuwai kubebwa na Eden Hazard tangu atue Chelsea mwaka 2013 akitokea Lille ya Ufaransa.

Mabadiliko; Katika mchezo wa leo, kocha Antonio Conte aliuanza kwa kutumia mfumo wa 3-5-2 huku kwenye safu ya ulinzi akiwatumia Cesar Azpilicueta, Gary Cahill na Antonio Rudiger wakati kwenye mchezo uliopita dhidi ya Newcastle alimtumia Andreas Christensen badala ya Rudiger wakati kwenye safu ya kiungo akiwatumia Victor Moses, Tiemoue Bakayoko, Cesc Fabregas, N'Golo Kante na Marcos Alonso.

Hitimisho; Chelsea inafanikiwa kushinda taji lake pekee kwa msimu huu huku ikiendeleza rekodi ya kuibamiza United kwenye uwanja huo wa Wembley mara mbili mfululizo katika hatua hiyo ya fainali. Ilipata ushindi pia kwenye fainali ya mwaka 2007 kwa goli 1-0 lililofungwa na Didier Drogba.

No comments:

Post a Comment