Nyota wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard anatajwa kuwa kwenye orodha ya makocha 100 wanaowania nafasi ya ukocha kwenye klabu ya Ipswich Town inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza.
Frank Lampard anatajwa kuwa kwenye orodha hiyo ya watu wanaowania nafasi ya ukocha klabuni hapo ambayo iliachana na kocha wake mwaka huu ikiwa imesalia michezo minne ili ligi hiyo kumalizika. Kwa taarifa zilizopo gwiji huyo wa Chelsea tayari ameshafanya mahojiano na mmiliki wa klabu hiyo, Marcus Evans.
Kocha rasmi anatarajiwa kutangazwa mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao, mwezi Juni.
Frank Lampard ambaye amekua akifanya kazi ya uchambuzi kwenye televisheni ya BT Sport amekuwa kwenye mafunzo ya ukocha ambapo kwa sasa ana leseni A ambayo inamruhusu kufundisha klabu yoyote isiyoshiriki mashindano ya Ulaya kama klabu bingwa Ulaya (Uefa Champions League) au ligi ya Ulaya (Europa League).
Labda Chelsea kwenye ligi kuu ingemaliza kwenye nafasi isiyoipa nafasi ya kufudhu michuano ya Ulaya kwa msimu ujao basi nyota huyu angeweza kuajiriwa kocha mkuu klabuni Chelsea kutokana na leseni yake.
Lakini pia hii inawezekana kuwa njia nyepesi ya kuinoa Chelsea kama mwenyewe anavyotamani ambapo kama akipata nafasi ya kuifundisha Ipswich basi atapata uzoefu wa kufanya kazi kama kocha mkuu lakini pia akiwa huko ataweza kujiendeleza kwenye leseni ili aweze kupata kibali cha kufundisha klabu inayoshiriki michuano yoyote.
No comments:
Post a Comment