Mfungaji bora wa muda wote klabuni Chelsea, Frank Lampard amefichua siri ambayo labda wengi hatukuijua juu ya Chelsea kushinda vita ya kumnasa nyota raia wa Ujerumani, Michael Ballack ambaye mwaka 2006 alitua Chelsea akitokea Bayern Munich ya nchini kwao Ujerumani.
Katika mahojiano aliyofanyiwa Lampard ambaye kwa sasa ni mmoja wa wachambuzi kwenye televisheni ya BT Sport ambapo alisema yeye ndiye alimfata mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich na kumweleza sifa nyingi kumhusu Ballack akisema uwezo wake mkubwa kama kiungo unamvutia kwa kiasi kikubwa na anaamini ni kiungo aliyekamilika na muda mfupi baadae Roman Abramovich akakamilisha usajili wa mjerumani huyo.
"Kukamilika kwa usajili wa Ballack sikuamini ni kutokana na maneno yangu, ila nadhani maneno yangu yalikuwa sababu mojawapo ya kusajiliwa kwake. Hakuna asiyeujua ubora wake, niliamini kama akitua Chelsea atacheza kwa kupambana sana" alisema mchezaji huyo wa zamani klabuni Chelsea.
Na alipoulizwa juu ya mahusiano yake na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich, Lampard alisema sijawai kuwa karibu na kiongozi mkubwa kwenye klabu kama nilivyokua karibu na Abramovich. Nilipokua West Ham ilikuwa unaweza kukaa muda mrefu bila kuonana na mmiliki, hata kwa Ken Bates (mmiliki wa Chelsea kabla ya Abramovich) hakuwa karibu sana lakini toka nimefika Chelsea, Abramovich alitufanya kuwa karibu yake, aliweza kutukumbatia na kutupongeza hata tunapopata ushindi wa 1-0 tukiwa nyumbani.
Frank Lampard aliondoka Chelsea mwaka 2013 na amekuwa akirejea klabuni hapo akijaribu mara kadhaa kuwafundisha wachezaji wa kikosi cha vijana.
No comments:
Post a Comment