Nyota wa Chelsea raia wa Hispania, Alvaro Morata anatajwa kutaka kuondoka klabuni hapo licha ya kuichezea kwa msimu mmoja toka ajiunge nayo kwenye dirisha kubwa la usajili la mwaka 2017 akitokea Real Madrid kwa dau la paundi milioni 60.
Nyota huyo anatajwa kutamani kurejea nchini Italia ambapo huko aliwai kucheza kwa mafanikio kwenye klabu ya Juventus kabla ya kurudi Real Madrid na baadae kutua Chelsea.
Alianza vyema klabuni Chelsea huku akifunga magoli nane kwenye michezo nane ya mwanzo lakini baadae akaonekana kuporomoka kwenye ubora wake huku akifunga magoli matatu tu toka siku ya ufunguaji zawadi (boxing day) mwaka jana.
Nyota huyo anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na viongozi wa klabu ya Ac Milan ya nchini Italia ambapo huko wanatafuta wachezaji wenye uwezo wa kucheza kama washambuliaji na tayari wameanza mazungumzo ya kumnasa mhispania huyo.
No comments:
Post a Comment