Nyota wengine kutoka Chelsea waitwa kombe la dunia - Darajani 1905

Nyota wengine kutoka Chelsea waitwa kombe la dunia

Share This

Ni siku kadhaa zimesalia kabla ya kuanza michuano ya kihistoria ya kombe la dunia itakayoanza mwezi Juni mwaka huu huko nchini Urusi.

Kuelekea kwenye michuano hiyo kila timu ya taifa imekua ikichagua wachezaji wake 23 watakaioziongoza timu zao za taifa kushiriki kwenye michuano ya kombe la dunia.

Kutoka Chelsea wameshaitwa wachezaji kama Eden Hazard, Thibaut Courtois pamoja na Michy Batshuayi ambao wote ni wabelgiji, Gary Cahill na Ruben Loftus-Cheek ambao wameshaitwa Uingereza, N'Golo Kante na Olivier Giroud ambao wameshaitwa Ufaransa wakati Willian Borges da Silva akiitwa Brazil lakini wengine pia walioitwa ni Cesar Azpilicueta ambaye ameitwa Hispania pamoja na Willy Caballero ambaye naye ameshaitwa Argentina.

Kwa kila kitakachokua kinaendelea juu ya wachezaji wa Chelsea walioitwa kuzitumikia timu zao kwenye kombe la dunia basi blog yako ya Darajani 1905 itakujuza mengi

No comments:

Post a Comment