Moja ya magwiji klabuni Chelsea, John Terry aliwai kuulizwa juu ya ubora na uwezo wa kijana huyu ambapo alitoa sifa nyingi na kubwa akiamini anaweza kuwa moja ya watu imara na muhimu hapo baadae. Amekuwa ni siri ya mafanikio kwenye timu ya vijana wa Chelsea wenye umri chini ya miaka 18 ambapo ameiongoza klabu hiyo kushinda mataji manne huku ikifika fainali ya klabu bingwa kwa vijana ambapo walipoteza mbele ya Barcelona.
Ni Trevoh Chalobah, kijana raia wa Uingereza mwenye miaka 18, ameweka rekodi mpya klabuni Chelsea mara baada ya juzi kuwa mmoja wa wachezaji kwenye kikosi kilichotwaa taji la kombe la FA ikiibamiza Man utd kwa goli 1-0 kwenye uwanja wa Wembley.
Nyota huyo ambaye ni mdogo wa mchezaji wa zamani wa Chelsea ambaye aliuzwa na kutimkia Watford, Nathaniel Chalobah amefanikiwa kuweka rekodi hiyo akiwa mchezaji aliyebeba kombe hilo mara nyingi kuliko nyota wengine nchini Uingereza. Nyota kama Kevin de Bruyne wa Manchester city, Mohammed Salah wa Liverpool pamoja na Harry Kane wa Tottenham ambao wote hawajawai kulibeba taji hilo wamezidiwa na kinda huyo ambaye hajacheza sekunde hata moja kwenye kikosi cha Chelsea FC lakini akitumika kama mchezaji wa akiba lakini akilitwaa mara moja.
No comments:
Post a Comment