Kocha mpya wa Chelsea awataka wachezaji watano - Darajani 1905

Kocha mpya wa Chelsea awataka wachezaji watano

Share This

Chelsea inaweza ikaachana na kocha wake Antonio Conte kama tetesi zinavyoeleza kwenye magazeti mengi barani Ulaya, kuisaidia klabu hiyo kushinda taji la kombe la FA bado hakuufanyi msimu wa pili wa kocha huyo klabuni Chelsea kuwa mzuri haswa pia kuifanya klabu hiyo kushindwa kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa msimu ujao ndio kunazidi kuchochea moto wa kocha huyo kuondoka.

Mchambuzi wa michezo ambaye anafanya kazi kwenye mtandao wa Chelsea, Pat Nevin anaamini kama Chelsea itakuwa chini ya kocha mwengine msimu ujao au ata kama itaendelea kusalia na kocha wake wa sasa basi ni lazima ihakikishe inawabakiza wachezaji wake watano wasiondoke klabuni hapo.

Mchambuzi huyo anaamini nyota hao ni lazima wabaki kama klabu hiyo inahitaji kupata mafanikio ikiwa chini ya kocha mpya.

"Sikuwa na ubishi nilipoona (Antonio} Rudiger alipochaguliwa kuwa nyota wa mchezo wa faimali dhidi ya Man utd pale Wembley. Ninaamini kama kuna mshambuliaji atakayecheza dhidi ya Rudiger basi atapata tabu sana. Amekua msaada mkubwa sana kwenye safu ya ulinzi ya Chelsea" alisema mchambuzi huyo ambaye alishawai kupita Chelsea kama mchezaji.

Nyota wengine waliotajwa na mchambuzi huyo kwamba kocha mpya anayekuja anatamani awakute ili aweze kuisaidia klabu hiyo kushinda mataji ni pamoja na Cesar Azpilicueta, N'Golo Kante, Thibaut Courtois pamoja na Eden Hazard.

No comments:

Post a Comment