Klabu ya Chelsea yakamilisha mpango wake wa kubadili jina - Darajani 1905

Klabu ya Chelsea yakamilisha mpango wake wa kubadili jina

Share This

Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea iliyokua ikitambulika kama Chelsea Ladies sasa imetangaza kubadili jina hilo na kutumia jina la Chelsea FC Women.

Klabu hiyo ya wanawake ilianzishwa mwaka 1992 lakini ilijumuishwa rasmi kuwa chini ya klabu ya Chelsea mwaka 2004 imekua ikitumia jina hilo la Chelsea Ladies kabla ya kutambulisha ubadilishaji wake leo hii.

Mwenyekiti wa Chelsea, Bruce Buck alisema "Tunaamini hii ni hatua kubwa na nje katika kufikia mapinduzi ya soka la wanawake haswa kwa klabu yetu. Tunajivunia kwa mafanikio waliyoyafikia na kuendelea kuyafikia kila siku ambapo hii inadumisha uimara na ubora wa soka la wanawake na wasichana".

Klabu hiyo imekua ikifanya pia michezo kwa wasichana ili kusaka na kutengeneza wachezaji wanawake ambao wanajumuishwa kwemye akademi ya Chelsea.

Kocha wa kikosi hicho cha wanawake, Emma Hayes naye alitoa neno juu ya hatua hiyo ya kuelekea mafanikio ambapo alisema "Hili jina litabadilisha mengi na kuleta radha mpya  na kulifanya soka la wanawake kuwa kwenye sayari au kampeni nyengine mpya ya kufikia mafanikio. Chelsea inaendelea kuonyesha kwa kiasi gani inajali na kuzingatia hali na nguvu ya klabu yetu. Nami nakubali mabadiliko haya" alisema mwanamama huyo ambaye alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume.

Klabu hiyo ya wanawake imefanikiwa kushinda mataji mawili ambayo ni kombe la FA ilipoibamiza Arsenal kwa magoli 3-1 kwenye fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Wembley lakini pia taji la ligi kuu Uingereza kwa wanawake ambalo linaitwa FA WSL huku ikifanikiwa kufika kwa mara ya kwanza nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment