Sarri aachana na Napoli, akaribia kusaini Chelsea - Darajani 1905

Sarri aachana na Napoli, akaribia kusaini Chelsea

Share This

Kocha wa klabu ya Napoli, Maurizzio Sarri ameachana na klabu hiyo ya nchini Italia na muda wowote kuanzia sasa anaweza akasaini mkataba wa kuinoa Chelsea kuanzia msimu ujao.

Maurizzio Sarri amekataa kusaini mkataba mpya klabuni Napoli na tayari imeshatolewa taarifa na rais wa klabu hiyo ya Napoli kuhusu kuondoka kwa kocha huyo. Rais wa klabu hiyo alitoa ujumbe ulieleza shukrani zake kwa kocha huyo kwa kuifanya Napoli ifikie mafanikio iliyoyafikia kwa aina ya uchezaji alioufikisha klabuni hapo.

Gazeti la barani Ulaya limeeleza kuna uwezekano kocha huyo akasaini mkataba klabuni Chelsea ndani ya masaa 48 yajayo.

No comments:

Post a Comment