Nyota wa Chelsea, Alvaro Morata ameonekana nchini Italia akiwa pamoja na wakala wake pamoja na kiongozi wa Juventus, Fabio Paratici.
Morata ambaye kwa sasa ana miaka 26 anatajwa kukaribia kuondoka Chelsea licha ya kujiunga nayo kwenye dirisha kubwa la usajili la mwaka jana akitokea Real Madrid kwa dau la paundi milioni 60 lakini ameshindwa kuendeleza makali aliyoanza nayo mwanzoni mwa msimu akiifungia Chelsea magoli nane kwenye michezo nane ya mwanzoni mwa msimu wakati mpaka sasa ameifungia magoli matatu toka tarehe 26-Februari.
Nyota huyo anatajwa kutua nchini Italia ili kukamilisha mipango ya usajili ya kutaka kujiunga nayo ambapo hiyo inaweza kuwa tiketi kwa klabu ya Chelsea kuendeleza nia yake ya kumnasa mshambuaji wa Bayern Munich, Roberto Lewandowski ambaye anatajwa kutakiwa na Chelsea.
No comments:
Post a Comment