Nyota wa zamani wa Chelsea, John Terry ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza ataiongoza klabu yake hiyo kucheza mchezo wa fainali ya kufudhu kugombania dhidi ya Fulham jumamosi hii ambapo mshindi wa mchezo huo ataungana na klabu mbili zilizomaliza kwenye nafasi ya kwanza na ya pili ili kushiriki ligi kuu Uingereza kwa msimu ujao.
Lakini mkataba wa nyota huyo anamaliza mkataba wake aliosaini kuitumikia klabu hiyo mwezi Juni mwaka huu ambapo alisaini mwaka mmoja pindi alipojiunga na klabu hiyo katika dirisha kubwa msimu uliopita.
Swali lililokua linawachanganya wengi vichwani mwao ni je atakubali kucheza dhidi ya klabu yake ya zamani? Chelsea? wakati sababu iliyomfanya akachagua klabu inayoshiriki ligi ya chini na inayoshiriki klabu yake pendwa ya Chelsea ni kutotaka kucheza dhidi ya klabu hiyo ambayo aliitumikia kwa miaka 22 akiichezea michezo 717.
Kocha wa klabu yake ya Aston Villa, Steve Bruce amesema anatamani mchezaji huyo asaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia klabu hiyo na kama tatizo ni kucheza dhidi ya Chelsea basi yupo tayari kutomjumuisha kwenye kikosi wakati Chelsea itakapocheza dhidi ya Aston Villa kama timu hiyo itafanikiwa kufudhu.
John Terry ambaye mpaka sasa ameshaitumikia Aston Villa kwenye michezo 32 amekua msingi imara kwenye mafanikio ya klabu hiyo huku akiwa pia kama nahodha wa klabu hiyo, madaraka aliyopewa tangu ajiunge nayo.
Lakini pia John Terry naye aliwai kuulizwa juu ya swala hili nae alisema yupo tayari kucheza dhidi ya Chelsea kwa kuwa toka amejiunga na Aston Villa amekua akipokelewa vibaya na mashabiki wa klabu hiyo huku wakionyesha kumuunga mkono kwa uwepo wake klabuni hapo kwa hivyo haoni ubaya kurudisha fadhila kwa mashabiki wa klabu hiyo ingawa mapenzi yake na Chelsea hayatokuja kufa milele.
No comments:
Post a Comment