Kocha Antonio Conte ni kama haonekani kuendelea kuwa kocha wa klabu hiyo kwa msimu ujao licha ya kuisaidia klabu hiyo kushinda kombe la FA mara baada ya kuifunga Manchester united kwa bao 1-0 lililofungwa na Eden Hazard kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Wembley.
Magazeti na vyombo vingi vya habari havimuoni wala kutegemea kocha huyo kusalia klabuni hapo ambapo mchezaji wa zamani wa Arsenal ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa soka lakini pia ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Thierry Henry ameelezea nafasi ya kocha huyo kusalia klabuni hapo kwa kusema anaziona siku za kocha kusalia klabuni hapo zinahesabika.
Kocha anayehusishwa kwa karibu kumrithi Antonio Conte klabuni Chelsea, Maurizzio Sarri ameachana rasmi na klabu aliyokua anaifundisha, klabu ya Napoli na sasa anatajwa kwa karibu kusaini mkataba mpya wa kuinoa Chelsea kuanzia msimu ujao
No comments:
Post a Comment