HAZARD KUTIMKIA MADRID KISA NYOTA WA MADRID - Darajani 1905

HAZARD KUTIMKIA MADRID KISA NYOTA WA MADRID

Share This
Klabu ya Real Madrid imekuwa ikimfukuzia nyota wa Chelsea, Eden Hazard kwa karibu ikiwa na mpango wa kumtumia nyota huyo ili kukiimarisha kikosi chake ambacho kinaonekana kuwa dhaifu sana msimu huu. Klabu hiyo imekuwa ikitajwa mara kadhaa kujaribu kuishawishi Chelsea iwauzie nyota huyo mwenye miaka 27 kwa kutaka kufanya mabadilishano ya wachezaji, ambapo wachezaji kama Isco, Marco Asensio na Gareth Bale wamekuwa wakitajwa kutumika katika mabadilishano hayo.

Na sasa nyota Gareth bale anatajwa kuvutiwa na mpango huo wa kutumika kama mabadilishano kati yake na nyota Eden Hazard ili mbelgiji huyo ajiunge na Madrid wakati yeye akijiandaa kutua klabuni Chelsea.

Vyanzo vya kuaminika vinadai kuwa Gareth Bale aliyesajiliwa na klabu hiyo kwa dau la dunia akiwa kama mchezaji ghali kwa kipindi iko akitoka Tottenham na kujiunga na wababe hao amekubali kurudi London ili ajiunge na Chelsea kutokana na nafasi yake kuonekana kuwa ngumu kwenye kikosi cha Real Madrid ambapo alikuwa nje kwa muda mrefu akisumbuliwa na majeraha, na sasa amerudi uwanjani na kuonekana hana furaha klabuni hapo na kuamua kuondoka klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment