THIBAUT COURTOIS AANZA MAZUNGUMZO, KUTIMKA AU KUBAKI? - Darajani 1905

THIBAUT COURTOIS AANZA MAZUNGUMZO, KUTIMKA AU KUBAKI?

Share This
Mlinda mlango wa Chelsea, Thibaut Courtois amekuwa akitajwa sana na vyombo vya habari akihusishwa kuondoka klabuni hapo na huku mwenyewe akikaririwa akisema moyo wake upo Madrid, jiji ambalo klabu ya Real Madrid inapattikana.

Nyota huyo inadaiwa amefanya mazungumzo na klabu ya nchini Ufaransa ambayo ni klabu tajiri iliyojichimbia kwenye jiji la Paris, Paris Dt.Germain (PSG) ili atimkie klabuni hapo. Nyota huyo anatajwa kufanya mazungumzo na klabu hiyo ili aungane nayo tofauti na ilivyokuwa ikitajwa mwanzo kwamba kuna uwezekano mkubwa akaungana na Real Madrid.

Nyota huyo mwenye miaka 25, familia yake ya mke pamoja na watoto wawili inaishi nchini Hispania kwenye jiji la Madrid ambapo hiyo ndio imekuwa ikitajwa kuchochea usajili wa mbelgiji huyo kuungana na klabu ya Real Madrid lakini sasa gazeti la nchini kwao Ubelgiji linaeleza nyota huyo ameanza mazungumzo na PSG na sio Real Madrid kama ilivyokuwa ikielezwa mwanzoni.

No comments:

Post a Comment