WACHEZAJI WA CHELSEA WAKASIRISHWA NA MORATA - Darajani 1905

WACHEZAJI WA CHELSEA WAKASIRISHWA NA MORATA

Share This
Gazeti moja la nchini Uingereza limeripoti kuwa wachezaji wa Chelsea wanachukizwa na kiwango anachokionyesha nyota ghali wa klabu hiyo, Alvaro Morata anayecheza nafasi ya ushambuliaji. Gazeti hilo linaeleza kuwa mara baada ya mchezo uliopita kati ya Chelsea iliyopoteza ugenini dhidi ya Manyumbu (Man utd), wachezaji wa Chelsea walimlalamikia nyota huyo raia wa Hispania kwa kuwa mwepesi na kuanguka kila anapoguswa na kupoteza nafasi za wazi.

Gazeti hilo linaeleza kwa sasa kwenye vyumba vya michezo wachezaji wa klabu hiyo hawaonekani kukubaliana na nyota huyo katika hali yake ya kushindwa kupambana na kuwa mwepesi kudondoka. Nyota huyo alianza msimu vizuri akifunga magoli sita katika michezo sita ya mwanzo lakini katika miezi kadhaa iliyopita kiwango chake na uimara wake unaonekana kuporomoka na kushindwa kupambana.

Nyota huyo alisajiliwa kwenye dirisha kubwa lililopita la mwezi Agosti kwa dau la paundi milioni 60 akitokea kabu ya nchini Hispania, Real Madrid.

No comments:

Post a Comment