COURTOIS KUONDOKA CHELSEA? MSIKIE WAKALA WAKE - Darajani 1905

COURTOIS KUONDOKA CHELSEA? MSIKIE WAKALA WAKE

Share This
Mchana wa leo kulisambaa taarifa zikimhusisha mlinda mlango wa Chelsea, Thibaut Courtois ambaye ni raia wa Ubelgiji zikisema nyota huyo aefanya mazungumzo na viongozi wa klabu ya Ufaransa, PSG ili msimu ukiisha auingane na klabu hiyo ingawa mwisho wa siku mazungumzo yakasimamishwa kwanza, ripoti hiyo ikitolewa na gazeti la nchini kwao Ubelgiji.

Lakini wakala wa nyota huyo amekuja hadharani na kusema taarifa hizo sio za kweli na kama kungekuwa na mazungumzo hayo basi angepewa taarifa yeye kama wakala wa nyota huyo.

"Sijasikia taarifa zozote kuhusu mazungumzo hayo. Kama klabu yoyote ikiwa na nia ya kumsajili (Courtois) wanajua nini cha kufanya, kukutana kwanza na klabu yake ili kukubaliana, kisha wafate kwangu. RTBF ni chobo kidogo nchini Ubelgiji, muda mwengine wanapenda kutumia habari kubwa kama hizi wakijua watapanda. Lakini taarifa hizo hazina ukweli wowote." alisema wakala huyo anayejulikana kwa jina la Christophe Henrotay.


Thibaut Courtois amekuwa akitajwa kwa karibu kuondoka klabuni Chelsea huku klabu inayohusishwa kumuwania kwa karibu ikitajwa ni Real Madrid ingawa PSG na wao wanaonekana kuvutiwa nae.

No comments:

Post a Comment