CONTE KUMPA NYOTA WAKE MKATABA MPYA - Darajani 1905

CONTE KUMPA NYOTA WAKE MKATABA MPYA

Share This
Klabu ya Chelsea inampango wa kujiimarisha zaidi katika kikosi chake kabla ya kumaliza msimu ili kuweza kupata nafasi ya kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, na hivyo haitaki kumpoteza nyota wake ambaye anacheza nafasi ya mlinda mlango namba tatu wa kikosini hapo, Eduardo mwenye miaka 35.

Taarifa zinadai kuwa Chelsea inaandaa kumpa mkataba mlinda mlango huyo raia wa Ureno, mkataba wa mwaka mmoja ili aendelee kusalia klabuni hapo.

Mlinda mlango huyo hajafanikiwa kupata nafasi ya kucheza mchezo wowte wakiushindani klabuni hapo lakini amekuwa na ushirikiano mzuri mazoezini ambapo amekuwa akiwa karibu na makipa wenzake Thibaut Courtois pamoja na Willy caballero na hivyo kuonekana kuna maana kubwa ya kuendelea kumbakisha klabuni hapo huku pia kukiwa na taarifa kuwa klabu mojawapo ya nchini kwao imepanga kumsajili mlinda mlango huyo na kumpatia nafasi kama mlinda mlango nambari moja klabuni kwao.

No comments:

Post a Comment