KITAMBO; GWIJI WA CHELSEA ANOGESHA UTAMU WA CHELSEA vs BARCA - Darajani 1905

KITAMBO; GWIJI WA CHELSEA ANOGESHA UTAMU WA CHELSEA vs BARCA

Share This
Leo ni moja kati ya siku kubwa katika historia ya soka duniani, wababe wawili watashuka uwanjani kupambana na kutafutwa nani atafanikiwa kufudhu kucheza hatua nyengine ya nane bora au robo fainali kati ya Chelsea dhidi ya Barcelona pale kwenye uwanja wa Stamford Bridge, ambapo mchezo huo ni hatua ya 16 bora kwa mchezo wa kwanza wa klabu bingwa barani Ulaya.

Lakini wakati Chelsea ikiwa inashuka uwanjani usiku wa leo, basi pia itakuwa inakumbuka siku ya kuzaliwa ya gwiji wa soka klabuni hapo, Peter Osgood ambaye alizaliwa siku kama ya leo miaka 71 iliyopita ingawa aliaga dunia akiwa na miaka 59, yaani alifariki miaka 12 nyuma (Mwaka 2006).

Gwiji huyo wa soka alikuwa na historia kubwa klabuni Chelsea mpaka kutajwa moja ya wakongwe na magwiji wasiokuja kusahaulika klabuni Chelsea huku katika uwanja wa Stamford Bridge ikiwekwa sanamu yake. Alicheza Chelsea kwa vipindi viwili tofauti huku akicheza michezo 289 na kufunga magoli 105.

Roho yako ilazwe mahali pema peponi, Amen!

No comments:

Post a Comment