MOSES AANZA MWAKA KWA TUNZO YA MCHEZAJI BORA - Darajani 1905

MOSES AANZA MWAKA KWA TUNZO YA MCHEZAJI BORA

Share This
Winga wa Chelsea, Victor Moses leo ataiongoza klabu yake kupambana dhidi ya Barcelona katika hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, lakini katika kuelekea usiku huo winga huyo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Nigeria kwa mwaka 2018 akiwashinda nyota kutoka klabu ya leicester, Wilfred Ndidi na nyota kutoka klabu ya Lobi Stars, Anthony Okpotu.

Moses amekuwa na wakati mzuri klabuni Chelsea haswa akiwa chini ya kocha Antonio Conte akitimiza kuichezea Chelsea michezo 100 lakini pia akiiongoza klabu yake ya Chelsea kutwaa taji lake la pili kati ya misimu mitatu la ligi kuu Uingereza.

Lakini sio hapo tu, ameiongoza pia timu yake ya taifa ya Nigeria kufanikiwa kufudhu kucheza michuano ya kombe la dunia kwa mwaka 2018 ambapo michuano hio itafanyika uko nchini Urusi kuanzia mwezi Juni.

Hongera kwake Victor Moses.

No comments:

Post a Comment