HABARI MUHIMU KUELEKEA CHELSEA vs BARCELONA - Darajani 1905

HABARI MUHIMU KUELEKEA CHELSEA vs BARCELONA

Share This
Tulikuwa tunazihesabu miezi, wiki, siku na sasa tunahesabu masaa kabla ya mtanange mkali wa raundi ya 16  bora kutimua vumbi pale kwenye uwanja wa Chelsea, Stamford Bridge ambapo Chelsea itaikaribisha klabu ya Barcelona kumenyana katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya. Mtihani unaoonekana kuwa mgumu kwa Chelsea, ni jinsi ya kumzuia mshambuliaji hatari wa klabu hiyo ya nchini Hispania. Ila muhimu ni kocha Antonio Conte kuonyesha ana mipango mizuri ambayo atataka sio kwa kumzuia Messi tu, ila kuizuia klabu nzima isiweze kupata ushindi katika mchezo wa leo.

Hapa nakuletea habari muhimu zinazouhusu mchezo huo ambao Chelsea itahitaji ushindi ili kujiwekea nafasi nzuri ya kupita katika hatua hiyo kabla ya kusafiri na kwenda nchini Hispania katika mchezo wa marudiano utakaochezwa tarehe 14-Marchi.

Habari muhimu;
Chelsea; Kama alivyosema kocha Antonio Conte kuwa wachezaji Tiemoue Bakayoko na David Luiz wataukosa mchezo wa leo kutokana na majeruhi wakati kwa upande wa Marcos Alonso na Ross Barkley wao wameanza mazoezi na timu jana ili kujiandaa na mchezo huu ambao utakuwa kivutio kwa wengi wakiutazama mchezo huu ambao unatajwa kuwa ndio utakaovuta mashabiki wengi kutokana na ukubwa wa timu zote mbili.

Barcelona; Klabu hiyo ya nchini Hispania ilitoa orodha ya wachezaji 21 watakaojiandaa ili kucheza katika mchezo wa leo huku Dembele aliyekuwa akitajwa kuwa na majeruhi ya muda mrefu akiwa kwenye kikosi hicho, na anategemewa kuwepo kwenye mchezo wa leo huku kwa upande wa Phillipe Coutinho hatokuwepo kutokana na sheria za chama cha soka cha Ulaya (UEFA) kutomruhusu mchezaji kuzichezea timu mbili katika michuano hiyo kwa msimu mmoja. Alishaichezea Liverpumba (Liverpool) katika hatua ya makundi kabla ya kuungana na klabu hiyo.

Mwamuzi; Cuneyt Cakir, mwamuzi raia wa Uturuki ambaye kwa sasa ana miaka 41, amekuwa hana historia nzuri na wachezaji raia wa Uingereza haswa kutoka Chelsea akiwa amehusika katika matukio mawili akitoa kadi nyekundu kwa walinzi Gary Cahill katika mchezo wa fainali ya klabu bingwa ya dunia mwaka 2012 dhidi ya Corithians ambapo Chelsea ilipoteza fainali hiyo kwa goli 1-0, lakini pia akihusika kwenye mchezo  kati ya Chelsea dhidi ya Barcelona mwaka huohuo 2012, akitoa kadi nyekundu kwa John Terry na Chelsea kupita katika hatua hiyo ya nusu fainali kwa magoli ya jumla ya 2-3.

Rekodi; Chelsea imepoteza mchezo mmoja kati ya michezo tisa iliyokutana dhidi ya Barcelona huku nyota wao Lionel Messi akiwa na rekodi mbaya dhidi ya Chelsea kwa kuwa timu ambayo hajawai kuifunga katika michezo nane aliyokutana nayo, huku akikosa mpaka mkwaju wa penati mwaka 2012.

Mechi zilizopita;
Chelsea; WLLWW
Barcelona; WDWDW

Muda; Saa 10:45 usiku (Saa 22:45)

No comments:

Post a Comment