MTOTO WA DROGBA AANZA KUFANYA MAKUBWA KAMA BABA YAKE - Darajani 1905

MTOTO WA DROGBA AANZA KUFANYA MAKUBWA KAMA BABA YAKE

Share This
Kupitia mtandao wa Instagram, nyota wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba ambaye alipata mafanikio makubwa klabuni Chelsea na mpaka sasa kuwa mwekezaji na mmiliki wa taasisi alituma ujumbe kupitia mtandao huo kuonyesha kufurahishwa kwake kwa mtoto wake kusajiliwa na klabu ya Guingamp ya nchini Ufaransa.

Mtoto wa gwiji huyo, Isaac Drogba amesajiliwa rasmi na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa. Didier Drogba alionyeshwa kufurahishwa kwake na mtoto wake huyo mwenye miaka 17 kwa sasa kujiunga na klabu hiyo ambayo baba yake pia alishawai kuichezea miaka 16 iliyopita na kufanikiwa kuichezea michezo 50 na kuifungia magoli 24.

Kupitia ujumbe huo, magwiji wenzake wa klabuni Chelsea, Frank Lampard pamoja na John Terry walionyesha kufurahishwa na taarifa hizo, ambapo kwa upande wa Frank Lampard aliandika "Namkumbuka Isaac, alikuwa kijana mdogo, leo amekuwa mbaba" huku kwa upande wa John Terry mwenyewe aliandika "Ni ngumu kuamini kwa kiasi gani amekua. Hongera"

Kinda huyo amejiiunga na klabu hiyo akitokea kwenye kikosi cha Chelsea cha akademi.

No comments:

Post a Comment