DROGBA ATAJWA MSHAMBULIAJI BORA - Darajani 1905

DROGBA ATAJWA MSHAMBULIAJI BORA

Share This

Nyota wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba ambaye kwa sasa anamiliki taasisi yake ya Didier Drogba Foundation ambayo inatoa misaada na kuihudumia jamii lakini pia ikihusika kwenye kuendeleza michezo kama mwenyewe alivyokuwa mwanamichezo ametajwa na gazeti au mtandao wa michezo wa FourFourTwo kama moja ya washambuliaji bora kuwai kutokea katika ligi kuu huku akiingia kwenye nafasi ya 8 katika orodha hiyo ya washambuliaji bora kuwai kuichezea ligi kuu Uingereza.

"Huwa ni ngumu sana kwa mchezaji kuwa sawa mara baada ya mashabiki wa timu yako kukuzomea na kukusema vibaya juu ya uchezaji wako. Drogba alipitia hali hiyo aliposajiliwa akitokea Marseille kwa paundi milioni 24 ambapo mwanzoni alikuwa akipigwa vita kabla ya kuamka na kuonyesha ubora wake na leo kuwa mmoja ya wakongwe wa Chelsea"

"Alikuwa kwenye kikosi kilichobeba mataji mawili ya ligi kuu mfululizo, kutoka msimu wa 2004-2005, na 2005-2006, lakini pia akawa mfungaji bora kwa magoli 29 huku akiiongoza Chelsea kuwa bingwa wa ligi kuu msimu wa 2009-2010, akaondoka hapo na kwenda China baadae akaenda Uturuki kabla ya kurudi tena Chelsea na kuiongoza kutwaa tena taji la ligi kuu kwa msimu wa 2014-2015."

"Kuwa mchezaji pekee kutoka Afrika kufunga magoli zaidi ya 100 ni rekodi inayodhihirisha kwa kiasi gani ni bora" kilisema chanzo hicho.

Angalizo; Mataji yaliyohesabika hapa ni kwa ligi kuu maana orodha hiyo ni kwa washambuliaji wa ligi kuu.

No comments:

Post a Comment