FABREGAS NA PEDRO WARUDI TENA BARCELONA - Darajani 1905

FABREGAS NA PEDRO WARUDI TENA BARCELONA

Share This
Imebaki siku moja ili dunia kushuhudia mtanange unaosubiriwa na kila mmoja mpenda michezo haswa mchezo wa soka. Imebaki siku moja ili dunia kupeleka macho yake kuangalia nini kitajiri pale katika uwanja wa Stamford Bridge unaopatikana Magharibi mwa jiji la London. Imebaki siku moja Chelsea kumenyana dhidi ya Barcelona ambapo mara ya mwisho kwa klabu hizo kukutana ilikuwa miaka sita iliyopita, ni nani atakuwa mjanja na shujaa safari hii mara baada ya safari iliyopita Chelsea kuibuka kuwa bingwa dhidi ya wababe hao na kufanikiwa kufudhu kucheza fainali ambapo huko walitoka kimasomaso kwa Chelsea kutwaa taji la ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich huko jijini Munich kwenye uwanja wao wa Allianz Arena.

Kuelekea kwenye mchezo huo ambao umebakiza siku moja, tayari shamrashamra na hamu ya kuuangalia mchezo huo ilishakuwepo ata kabla ya siku moja kufika, mpaka tunafikia kwenye siku moja, tayari tulishakuwa na siku saba, zikaja sita, tano na leo tumefikia kwenye hii siku moja.

Nyota wa Chelsea, Pedro Rodriguez pamoja na Cesc Fabregas ambao wote ni raia wa Hispania, nchi ambayo inatokea klabu hiyo ya Barcelona lakini pia walishawai kupita kwenye klabu hiyo na kupata mafanikio makubwa kwa sasa wote wapo Chelsea, na wamepata nafasi ya kufanya mahojiano na klabu yao hiyo ya zamani kupitia kwenye chaneli yao ambayo ni maalumu kwa ajili ya klabu hiyo wakihojiwa juu ya nini wanakiona tofauti na walipokuwa klabuni Barcelona na sasa kuwepo klabuni Chelsea.

Walihojiwa mambo mengi, lakini kikubwa walipata fursa ya kuwa kwenye chaneli ya klabu hiyo ya zamani ambapo kesho watakuwa wanacheza dhidi yao klabuni Chelsea. Mpira sio vita, soka hudumisha amani na ndio maana na wao wakapata kibali kutoka kwa uongozi wa Chelsea kufanya mahojiano hayo.

Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Darajani 1905 tumeshindwa kukuletea mahojiano ya nyota hao walipokuwa na chaneli hiyo, lakini kikubwa ni kuonyesha soka safi na sisi kama mashabiki wakubwa wa Chelsea tunategemea kupata

No comments:

Post a Comment