ASENSIO AITISHIA KLABU YAKE, ATAKA KUTUA CHELSEA - Darajani 1905

ASENSIO AITISHIA KLABU YAKE, ATAKA KUTUA CHELSEA

Share This
Chelsea imekuwa ikitajwa kumfukuzia nyota wa klabu ya Real Madrid, Marco Asensio ambaye anatajwa kuwa moja ya nyota watakaokuja kung'aa sana kwenye soka baada ya miaka kadhaa, lakini inaeleweka kuwa klabu hiyo ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu Hispania pamoja na klabu bingwa Ulaya watataka kumtumia nyota huyo kama mabadilishano ili kumnasa Eden Hazard kutoka Chelsea.

Lakini kwa upande wa nyota huyo anatajwa kutoa onyo kwa viongozi wa klabu yake kutokana na kutokuwa na uhakika wa kupata nafasi katika kikosi cha Real Madrid na hivyo kuwaambia kama hatoendelea kupata nafasi basi ana ofa nyingi za kutoka vikubwa duniani ambavyo vinahitaji huduma yake kwa maana hiyo ataweza kuondoka klabuni hapo.

Marco Asensio anatajwa kuwa kikubwa cha mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ambaye alipokea ushauri kutoka kwa watu wa karibu kuwa akubali kumtumia Eden Hazard ili ajiunge na Real Madrid ili ampate nyota huyo pamoja na fungu nono la pesa ambalo Real Madrid wanatajwa kuwa tayari kulitoa.

Taarifa zinadai kuwa kutokana kwa nyota huyo kutopata nafasi kikosini Real Madrid, naye anashinikiza kocha wake Zinedine Zidane aondoke klabuni hapo ambapo kuondoka kwa kocha huyo kunachochewa pia na kuwa na msimu mbovu akiachwa alama 17 na wapinzani wao wakubwa, Barcelona ambao wapo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Hispania.

No comments:

Post a Comment