MSIKIE MKONGWE WA SOKA ANACHOKISEMA KUHUSU HAZARD - Darajani 1905

MSIKIE MKONGWE WA SOKA ANACHOKISEMA KUHUSU HAZARD

Share This
Nyota wa Chelsea, Eden Hazard amekuwa akihusishwa kwa karibu kutakiwa na klabu ya nchini Hispania, Real Madrid ambao wenyewe wamekuwa wakimtaja nyota huyo raia wa Ubelgiji kama mtu sahihi kutua klabuni hapo ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho cha kocha raia wa Ufaransa, Zinedine Zidane.

Mara baada ya kuhusishwa na klabu hiyo huku kukiwepo taarifa juu ya nyota huyo kugoma kusaini mkataba mpya klabuni Chelsea ambapo baba yake Thierry Hazard alidai kugoma kusaini mkataba mpya kwa mtoto wake huyo ni ili kuifanya klabu ya Real Madrid iendelee kuongeza nguvu ili kumsajili.

Kutokana na fununu na taarifa hizo, mchezaji wa zamani wa Liverpumba (Liverpool), Jamie Carragher ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa soka amesema anaamini kama Chelsea itashindwa kufudhu kucheza klabu bingwa Ulaya kwa kumaliza nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi kuu Uingereza au kwa kuwa bingwa wa michuano hiyo ambapo itamaanisha atafanikiwa kucheza katika michuano hiyo msimu ujao kama bingwa mtetezi.

"Kwa kauli aliyoisema kuwa anaamini Chelsea ni klabu inayostahili kutwaa mataji basi itakuwa ngumu kwake kusalia hapo endapo Chelsea itashindwa kufudhu, kila klabu bora duniani inafatilia tukio hili, kama Chelsea ikishindwa kufudhu basi naamini kila klabu itapeleka nia yake ya kumsajili" alisema Carragher.

Je unakubaliana na uchambuzi huu?

No comments:

Post a Comment