KWA MWAMUZI HUYU, CHELSEA IWE MAKINI MBELE YA BARCA - Darajani 1905

KWA MWAMUZI HUYU, CHELSEA IWE MAKINI MBELE YA BARCA

Share This

Chelsea inaelekea kucheza mchezo wake muhimu wa hatua ya 16 bora katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona siku ya tarehe 20-Februari ambapo itakuwa ni jumanne usiku.

Kuelekea kwenye mchezo huo  ambapo atakayefanikiwa kuvuka kwenye hatua hiyo mara baada ya kucheza mchezo wa kurudiana tarehe 14-Marchi ambapo mshindi wa jumla atafanikiwa kufudhu kucheza hatua ya robo fainali, mwamuzi wa mchezo huo kati ya Chelsea dhidi ya Barcelona tayari ameshateuliwa na hapa nimekuletea habari hii ili kukujuza mambo muhimu kuhusu mwamuzi huyo raia wa Uturuki.

Anaitwa Cüneyt Cukar, mwamuzi raia wa Uturuki mwenye miaka 41 kwa sasa huku akiwa amehusika kuchezesha michezo mingi kama mwamuzi anayetambulika na chama cha soka duniani (FIFA) lakini pia akiwa na sifa ya kuchezesha michezo mingi ya watani wa jadi ambayo kwa Uturuki huwa ni michezo migumu, akichezesha mara tano kati ya Fenerbahce dhidi ya Galatasaray, lakini je wajua kuwa mwamuzi huyo huwa anatajwa kuwa na bahati mbaya na wachezaji raia wa Uingereza? lakini sio kwa wachezaji tu, ila hata kwa Chelsea?

Ndiyo, mwamuzi huyo amekuwa akitajwa kati ya marefa wagumu sana pale wachezaji wa kiingereza wanapokuwa uwanjani naye akawa mwamuzi, lakini pia huwa ana bahati mbaya zaidi na Chelsea ambapo katika michezo kadhaa ambayo aliichezesha uku Chelsea ikiwa uwanjani ameshatoa kadi nyekundu mara mbili katika michezo miwili tofauti. Alishampa John Terry kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Barcelona ambapo Chelsea ilifanikiwa kupata sare ya 2-2 ingawa Chelsea walikuwa pungufu na kufanikiwa kufudhu kucheza fainali kwa matokeo ya jumla ya mabao 2-3 hiyo ilikuwa mwaka 2012 katika hatua ya nusu fainali ya michuano hii ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Lakini pia aliwai kumtoa nje kwa kadi nyekundu mlinzi wa Chelsea, Gary Cahill katika mchezo ambao Chelsea ilikuwa ikimenyana dhidi ya Corithians katika mchezo wa fainali ya klabu bingwa ya dunia ambapo Chelsea ilipoteza mchezo huo.

Kuonyesha kuwa mwamuzi huyo huwa hanaga huruma haswa kwa wachezaji wa kiingereza, wakati timu ya taifa ya Uingereza yenye jina la utani la 'Three Lions' ilipokuwa inajiandaa kwenda kushiriki michuano ya Euro mwaka 2016, gazeti la Mirror la nchini Uingereza lilitoa makala kuhusu Uingereza kuwa macho na mwamuzi huyu ambaye alikuwepo kwenye orodha ya waamuzi wenye maamuzi magumu haswa kwa wachezaji wa Uingereza kama ilivyo kwa John Terry pamoja na Gary Cahill ambao nao ni waingereza.

Gazeti hilo lilikuwa likikumbushia matukio ya kadi nyekundu ambazo mwamuzi huyo alipotoa kwa wachezaji raia wa Uingereza ama kwa timu za Uingereza.

No comments:

Post a Comment