TOTTENHAM YAOGOPESHWA NA CHELSEA - Darajani 1905

TOTTENHAM YAOGOPESHWA NA CHELSEA

Share This

Chelsea imekuwa ikitajwa kwa hivi karibuni kumfukuzia mlinzi wa klabu ya Tottenham, Toby Alderwield ambaye ni raia wa Ubelgiji. Ambapo kumfukuzia nyota huyo kunaitisha klabu yake ikiona kuna dalili zote za nyota huyo kuondoka klabuni hapo katika dirisha kubwa la usajili linalokuja.

Toby amekuwa akicheza kwa mafanikio klabuni Tottenham, kabla ya klabu hiyo kufanikiwa kumnasa mlinzi kutoka klabu ya Ajax inayoshiriki ligi kuu nchini Uholanzi, Davinson Sanchez ambaye anatajwa kujenga ukuta imara katika safu ya ulinzi ya Tottenham huku akitajwa kuwa mmoja wa walinzi makinda wanaofanya vizuri kwa sasa.

Tottenham inaogopa kumpoteza Alderwield licha ya kuonekana hana nafasi kikosini hapo huku wakitishwa na Chelsea kuhusishwa kumtaka mlinzi huyo.

No comments:

Post a Comment