CHELSEA LADIES YAIBAMIZA DONCASTER - Darajani 1905

CHELSEA LADIES YAIBAMIZA DONCASTER

Share This

Timu ya wanawake ya Chelsea inayotumia jina la Chelsea Ladies imefanikiwa kupata ushindi jioni ya leo ikiibamiza klabu ya Doncaster ya wanawake wenzao kwa magoli 6-0.

Mchezo huo uliohudhuriwa na watazamaji 1564 ulianza kwa Chelsea Ladies kuzidiwa katika kumiliki mpira ingawa ilifanikiwa kupata goli moja lililofungwa na Ji So-Yun mwenye uraia wa Korea ya Kusini na kufanya Chelsea Ladies kutoka kimasomaso katika kipindi iko cha kwanza kwa goli 1-0.

Lakini kipindi cha pili kilikuwa ndicho kipindi cha Chelsea Ladies ambao walionyesha ubora wao kupitia kwa nyota wake tena Ji So-Yun ambaye alifunga magoli mawili katika kipindi iko akimalizia pasi murua za Fran Kirby na Drew Spence na kumfanya mkorea huyo kufunga magoli matatu yaliyomaanisha alikuwa tayari ameshafunga 'Hat-trick'.

Lakini bado haikutosha kwa nyota Erin Cuthbert aliyeingia kama mchezaji wa akiba na kufanikiwa kufunga magoli mawili yaliyomfanya kutimiza magoli 5 katika michuano hiyo ya kombe la FA kwa akinadada. Na goli la sita likakamilishwa na nyota mwengine Ramona Bechmann ambaye mwenyewe alifunga kwa mkwaju wa penati.

Kwa matokeo haya, yanamaanisha Chelsea Ladies inakaribia kufudhu katika raundi hiyo na kukaribia kuingia kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya kombe la FA kwa akina dada.

Hongereni dada zetu...

No comments:

Post a Comment