CONTE AELEZA MFUMO ATAKAOTUMIA KUMZUIA MESSI - Darajani 1905

CONTE AELEZA MFUMO ATAKAOTUMIA KUMZUIA MESSI

Share This

Chelsea itakuwa na kibarua kigumu siku ya jumanne ya tarehe 20-Februari ambapo itakuwa inawakaribisha wababe wa ligi kuu Hispania, Barcelona kucheza mchezo wake wa hatua ya 16 bora ya klabu bingwa Ulaya. Ambapo mchezo unatajwa kuwa mchezo mgumu na unaosubiriwa kwa hamu kuangaliwa siku hiyo.

Kocha wa klabu ya Barcelona, Ernesto Valverde jana alihojiwa mara baada ya mchezo wake dhidi ya Eibar ambapo alipata ushindi wa mabao 2-0, ushindi ambao umekuja mara baada ya klabu hiyo kupata matokeo ya sare mara mbili mfululizo katika ligi kuu. Kocha huyo aliulizwa juu ya maoni yake na alisema anaitazama Chelsea kawaida tu.

Kusoma alichokisema kocha huyo, bonyeza hapa

Lakini kwa upande wa kocha Antonio Conte, ambaye ni kocha wa Chelsea na alishawai kushinda taji hilo la ligi ya mabingwa Ulaya alipokuwa mchezaji mwaka 1996 akiwa na klabu ya Juventus, alipoulizwa juu ya kama Chelsea itaweza kumzuia mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi katika michuano hiyo, kocha huyo alisema "Natumaini tutaendeleza utamaduni huo (wa Messi kutokuifunga Chelsea katika michezo nane aliyokutana na Chelsea). Lakini nataka kurudia, tunamzungumzia mchezaji bora, tunatakiwa kumheshimu"

"Lakini pia wakati huohuo tunatakiwa kujaribu kuonyesha soka la kipekee kwa mchezo huu na kwa changamoto hii iliyopo mbele yetu"

"Tunamzungumzia (Messi) moja ya wachezaji bora duniani lakini nina uhakika, tunatakiwa kupambana pamoja kama timu na sio kumtegea mchezaji mmoja amzuie. Maana nachokifikiria kama tukitumia mfumo wa kumkabidhi mchezaji mmoja kumzuia basi ni lazima Messi atakuwa hatari kwetu" alisema kocha huyo.

Chelsea inahitaji ipate ushindi au matokeo yatakayoifanya iwe na faida kubwa na nafasi kubwa ya kuifanya isonge mbele katika michuano hiyo huku mchezo wa marudiano ukitajwa kufanyika tarehe 14-Marchi ambapo utachezwa uko nchini Hispania kwenye dimba la Camp Nou, na tiketi za mchezo huo zishaanza kuuzwa.

No comments:

Post a Comment