RUDIGER AGOMBANIA TUNZO UJERUMANI - Darajani 1905

RUDIGER AGOMBANIA TUNZO UJERUMANI

Share This

Mara baada ya kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante kuchaguliwa mchezaji bora wa mwaka nchini kwao Ufaransa kwa mwaka 2017, huenda mlinzi wa Chelsea, Antonio Rudiger naye akashinda tunzo nchini kwao Ujerumani.

Rudiger ambaye amesajiliwa na Chelsea huku akicheza msimu huu ambao ni msimu wake wa kwanza akisajiliwa kwa paundi milioni 34 kutokea klabuni As Roma ya nchini Italia ambapo huko alicheza soka safi na hata kuchaguliwa kwenye timu ya taifa iliyochaguliwa kwenda kwenye michuano ya kombe la mabara kwa timu ya Ujerumani kwa mwaka 2017 na kufanikiwa kutwaa taji hilo huku Rudiger akicheza michezo minne kati ya mitano na katika michezo hiyo ikiruhusu magoli manne tu.

Rudiger anashindania tunzo hiyo huku akishindana na nyota wenzake 11 huku akiwa mchezaji pekee kutoka Chelsea.

Orodha kamili: Marc-Andre ter Stegen (Barcelona), Joshua Kimmich(Bayern Munich), Mathias Ginter(Borussia Monchengladbach), Antonio Rudiger (Chelsea), Jonas Hector (FC Koln), Julian Draxler (PSG), Emre Can(Liverpool), Sebastian Rudy (Bayern Munich), Leon Goretzka (Schalke), Timo Werner (RB Leipzig), Lars Stindl (Borussia Monchengladbach)

No comments:

Post a Comment