Unadhani ni tukio gani linamfanya akumbukwe pale klabuni Chelsea kama sio goli lake la pekee alilolifunga dakika za majeruhi katika mchezo wa ligi kuu wakati Chelsea ilipokuwa ugenini kucheza dhidi ya West Bromwich pale kwenye uwanja wa Hawthorns.
Goli lake liliifanya Chelsea ijihakikishie ubingwa wa ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2016-2017.
Michy Batshuayi anatimiza miaka miwili hii leo toka kutua klabuni Chelsea akisajiliwa akitokea kwenye klabu ya Olympique Marseille huku akiigharimu Chelsea dau la paundi milioni 35.
Mpaka sasa ameshaichezea Chelsea michezo 36 na kuifungia magoli 9 huku kwa msimu uliopita aliutumia nusu msimu akiwa kwa mkopo kwenye klabu ya Borrusia Dortmund ambapo huko alifanikiwa kufunga magoli 9 katika michezo 14 aliyocheza.
Nyota huyo ambaye anajulikana pia kama 'Batman' likiwa ni jina lake la utani alilobatizwa haswa kutokana na mapenzi yake na filamu hiyo ya mapigano kwa sasa yupo nchini Urusi akiitumikia timu yake ya taifa ya Ubelgiji.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment