Leo nakuletea makala inayomhusu nyota kinda wa Chelsea, Reece James nyota kinda aliyelelewa na kukuzwa kwenye akademi ya Chelsea.
Mchezaji wa kwanza aliyekuwa anamtazama sana:
"Nilikuwa namtazama sana Didier Drogba, ni mchezaji niliyekuwa najifunza kutoka kwake kwasababu nilipokuwa mdogo nilikuwa nacheza nafasi ya mshambuliaji. Nilikuwa najifunza vingi kutoka kwake."
Viatu vya kwanza kuvichezea:
"Viatu vyangu vya kwanza viliitwa Predators, vilikuwa ni toleo maalumu kutoka Uefa Champions League. Lakini kama ilivyo kawaida kila unapoona viatu vipya unatamani kuvipata. Ata siku hizi mazoezini, akija mwenzetu na viatu vipya wote tunamfata tunavutiwa navyo."
Kumbukumbu yake ya kwanza kwenye soka;
"Nilipochukuliwa na akademi ya Chelsea. Ilikuwa kumbukumbu nzuri sana kwangu. Walinichagua kutokea kwenye ligi moja ya watoto nikiwa nna miaka sita, nilichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano nao wakavutiwa na uwezo wangu. Wakanichukua."
Taji la kwanza kushinda;
"Ilikuwa nikiwa nina miaka 10 au 11, nikiwa na kikosi cha akademi ya Chelsea tulienda jijini Venlo nchini Uholanzi, kulikuwa na mashindano. Fainali tulicheza dhidi ya Crub Brugge, hilo ndilo taji langu la kwanza. Jambo zuri nililofurahia nilikuwa mmoja kati ya wapiga penati, na nilifunga."
Timu ya kwanza kuichezea akiwa mdogo:
"Iliitwa Kew Park Rangers."
Jina lake la kwanza la utani:
"Wakati nikiwa nnakua sikuwai kuwa na jina la utani, lakini nilipoenda kwa mkopo Wigan wakaanza kuniita 'Jamo'
Kitu cha kwanza anachokifanyaga akishafika mazoezini:
"Naenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, nachukua 'chewing gum' kisha nachukua 'headphone' kisha naingia uwanjani."
Kama angekuwa kocha ni wachezaji gani angewasajili?
No comments:
Post a Comment