KUELEKEA CHELSEA vs BARCELONA, MSIKIE ASHLEY COLE ALICHOKISEMA - Darajani 1905

KUELEKEA CHELSEA vs BARCELONA, MSIKIE ASHLEY COLE ALICHOKISEMA

Share This
Unamkumbuka yule anayetajwa kuwa moja ya walinzi wa kushoto bora kuwai kutokea kwenye ligi kuu Uingereza? Ashley Cole, kwa sasa ana miaka 37 na bado anasakata kabumbu akiwa kwenye klabu ya LA Galaxy ya nchini Marekani. Wengi wetu tulikuwa tunamfananisha kwa majina na winga wa Chelsea, Joe Cole. Nakumbuka mimi mwenyewe nilikuwa nadhani ni ndugu kisa wamefanana majina ya ubin. Ila wote ulikuwa utoto maana tulianza kuipenda Chelsea bila kujua mpira ni nini.

Turudi kwenye maada, gwiji huyo ametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter kuhusu mchezo wa leo ambao Chelsea itakuwa nyumbani kumenyana dhidi ya Barcelona. Gwiji huyo ametuma ujumbe ulosomeka "Nimeshangazwa na mchezo wa Chelsea dhidi ya Barcelona utakaochezwa baadae alafu mi sitokuwa uwanjani (kama mchezaji wa Chelsea)😂Nimekumbuka kucheza mechi za klabu bingwa @ChelseaFC tunaweza kupambana"

Ashley Cole alicheza Chelsea kwa mafanikio makubwa huku usajili wake wa kutua Chelsea akitokea Arsenyani (Arsenal) ambapo mashabiki wa klabu hiyo walikasirishwa sana na mchezaji huyo kwa kutoka kwenye klabu yao na kuja Darajani. Lakini pia nyota huyo aliwai kucheza dhidi ya Barcelona ambapo alikuwepo kwenye kikosi kilichoitoa Barcelona na kutwaa taji la ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2012.


Je unakumbuka lipi kuhusu gwiji huyu?

No comments:

Post a Comment