UNATAMANI LAMPARD AWE KOCHA WA CHELSEA? SOMA ALICHOKISEMA - Darajani 1905

UNATAMANI LAMPARD AWE KOCHA WA CHELSEA? SOMA ALICHOKISEMA

Share This
Mwezi Februari mwaka 2017, Chelsea ilikuwa nyumbani mkukimenya katika mchezo wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Swansea, mchezo ulioisha kwa Chelsea kushinda 3-1 dhidi ya Swansea na kufanikiwa kuongeza pengo la alama 11 dhidi ya aliyekuwa anashika nafasi ya pili katika msiamo wa ligi kuu Uingereza. Lakini siku hiyo, gumzo halikuwa juu ya matokeo hayo, ila alichokiongea gwiji wa soka, Frank Lampard ambaye aliingia uwanjani wakati klabu zikiwa zimeenda mapumziko ambapo nyota huyo aliongea neno lake la asante kwa mashabiki wa Chelsea kwa kuwa nae na kuwa mkongwe klabuni hapo huku akiichezea klabu hiyo kwa miaka 13 na kufanikiwa kuwa mfungaji bora wa muda wote.

Aliongea maneno machache siku hiyo maana alitumia muda mwingi kuzunguka katika dimba la uwanja wa Stamford Bridge akisema asante na kuwashukuru mashabiki kwa kuwapungia mkono ambapo tukio hilo lilichukua muda mrefu kabla ya timu kurejea uwanjani kumalizia ngwe ya pili ya mchezo huo, lakini katika mambo aliyoongea alisema alikuwa anajutia kuondoka klabuni hapo bila kusema asante, na siku hiyo alirudi hapo ili kutimiza dhamira yake hiyo lakini huku akisema asingeweza kufikia alipofikia kama asingepata ushirikiano wa mashabiki wa Chelsea.

Tuachane na hayo yote, maana nilikuwa nataka nikuonyeshe kwa kiasi gani tunawakumbuka na kuwakosa wachezaji wenye moyo wa kuipenda kwanza klabu na sio wao kujiona wapo juu ya klabu kutokana na ubora wao.

Nyota huyo kwa sasa anajihusisha na mafunzo ya ukocha, na kuna uwezekano akapata timu na kuifundisha muda wowote kuanzia sasa maana ana leseni inayotambulika ya Daraja A, wengi wamekuwa wakitamani arudi ili aifundishe Chelsea, je wewe ni mmoja wao? msikie anachokisema mwenyewe.

"Leseni yangu ya daraja A nitaipata katika kipindi kifupi kijacho. Ambapo hiyo inamaanisha naweza kuanza kuifundisha klabu yoyote. Leseni ya ubora mkubwa zaidi nitaanza kuishughulikia kwenye kipindi cha kiangazi ambapo hiyo ndio itaniruhusu kufundisha timu mpaka kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya na michuano mikubwa ya Ulaya ambapo ili kuipata itanichkua mwaka mmoja"

"Naweza kufanya kazi kwenye klabu au timu yoyote, lakini sintoruhusiwa kushiriki michuano ya Ulaya. Kama kuna timu itataka tufanye kazi, nitaangalia" alisema gwiji huyo ambaye aliondoka Chelsea kama mchezaji mwaka 2014.

Nyota huyo amekuwa akihudhuria kwenye mazoezi na michezo ya klabu ya Chelsea ya vijana ambapo amekuwa akifanya kazi pia kama mwangalizi wa kikosi hicho cha vijana chini ya miaka 18.

No comments:

Post a Comment