CHELSEA HATIHATI KWA NYOTA WA AC MILAN - Darajani 1905

CHELSEA HATIHATI KWA NYOTA WA AC MILAN

Share This
Chelsea iliwai kumfukuzia nyota wa klabu ya Ac Milan, Allesio Romagnoli ambaye anaichezea klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Italia ambapo mwaka 2016 Chelsea iliwai kumtaka bila kufanikiwa. Na sasa inaelezwa kuwa imeanza mipango ya kumfukuzia nyota huyo kimyakimya kwa nia ya kuja kutengeneza ukuta wa ulinzi ili uzidi kuwa imara kutokana na baadhi ya wachezaji wa nafasi hiyo klauni Chelsea kuonekana umri kuwatupa mkono. David Luiz na Gary Cahill wote wana miaka zaidi ya 30.

Lakini klabu yake inaelezwa imeanza taratibu za kuanza mazungumzo ili kusaini mkataba mpya klabuni hapo ambapo amekuwa akitumika vyema sambamba na Leonardo Bonucci kujenga ukuta imara wa klabu hiyo ya Ac Milan na kufanikiwa kufudhu kucheza hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya Europa ambapo katika hatua hiyo ya 16 bora klabu hiyo imepangwa kukutana dhidi ya Arsenyani (Arsenal).

Chelsea inatajwa iliwai kupeleka dau la euro milioni 40 kwa klabu hiyo ili kumsajili mlinzi huyo mwenye miaka 23 kwa sasa ila dili hilo likapigwa chini na tajiri wa Ac Milan, Rossonerri.

No comments:

Post a Comment