NAINGGOLAN AELEZA SABABU YA KUSHINDWA KUTUA CHELSEA - Darajani 1905

NAINGGOLAN AELEZA SABABU YA KUSHINDWA KUTUA CHELSEA

Share This
Chelsea imekuwa ikitajwa mara kadhaa kumfukuzia nyota wa klabu ya nchini Italia, klabu ya As Roma ambaye ni raia wa Ubelgiji, Radja Nainggolan, lakini mara zote imekuwa ikipigwa chini juu ya kutaka kumsajili nyota huyo anayecheza nafasi ya kiungo klabuni hapo.

Katika kukosa kumnasa nyota huyo ambapo iliwai kuripotiwa kuwa moja ya viongozi wa Chelsea alikuwa akifanya nae mazungumzo ili asajiliwe, lakini mwisho wa siku hakuna kilichoendelea na nyota huyo bado yupo kwenye klabu yake ya As Roma na aliiongoza katika michezo miwili ambayo Chelsea ilicheza dhidi ya klabu hiyo katika michezo ya klabu bingwa Ulaya kwa hatua ya makundi.

Nyota huyo amefanyiwa mahojiano na kuulizwa ni nini kilimfanya ashindwe kutua Chelsea, nyota huyo alijibu akisema "Ningeweza kwenda Chelsea au klabu nyengine yoyote iliyonitaka lakini kuanza maisha mapya kwenye klabu mpya ukiwa na miaka 28 au 29 tena katika hali tofauti ya maisha? sio kwangu, hilo siwezi kulifanya"

"Napenda haswa kuwa sehemu nayojihisi vizuri na kuwa na uhuru zaidi. Kama mshahara mkubwa ungekuwa ndio chaguo langu au mapenzi yangu basi mpaka leo ningekuwa nimeshazichezea klabu nyingi, lakini mapenzi yangu sio mshahara mkubwa, ila kuwa sehemu nayoishi vizuri. Inatakiwa uishi vyema na ucheze mahali ambapo una furaha napo, nami vyote hivyo ninavyo"

"Kila kitu kipo sawa kwangu, na hata familia yangu ina furaha kuishi kwenye jiji hili la Roma. Kuna migahawa mizuri na maduka mengi nayoweza kufanya manunuzi ambayo hata familia au marafiki wakinitembelea tunaweza kujumuika pamoja" alisema nyota huyo.

No comments:

Post a Comment